Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya (NHIF) unakamilisha taratibu za uwekeza kwenye vifaa tiba
vitokanavyo na pamba na bidhaa za maji ya dripu(Infusion Fluids).
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati akijibu hoja
mbalimbali za wabunge mjini Dodoma.
“Gharama za miradi hii inakadiriwa
kufikia dola za kimarekani milioni 36.5 na kutoa ajira za moja kwa moja
1600 na zisizo za moja kwa moja 5000”, Alisema Mhe.Mwijage.
Amesema mradi huu unakadiriwa
kutumia pamba tani elfu 50 kwa mwaka na Serikali ya Mkoa wa Simiyu
inaendelea na jitihada za kutenga maeneo ya uwekezaji kwa kuwalenga
wajasiriamali wadogo,wa kati mpaka wakubwa bila kujali kama ni wa kutoka
ndani au nje ya nchi.
Aidha amesema kuwa azma ya
Serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda imeainishwa vyema katika mpango
wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2016/17-2020/21 wenye
dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na
maendeleo ya watu.
Pamoja na hayo ameainisha kuwa ili
kufikia azma hiyo ushiriki wa mchango wa mtu mmoja mmoja,makundi ya
watu,taasisi za umma na taasisi binafsi unahitajika.
Amebainisha mikakati minne ambayo
imeanza kufanyiwa utekelezaji ni ya ngozi,mafuta ya kula,nguo na mazao
jamii ya kunde uku wakati huohuo mpango wa wilaya moja,zao moja na
uhamasishaji wa ujenzi wa viwanda chini ya SIDO unaendelea nchini kote.
No comments:
Post a Comment