Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha nane
cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais (TAMISEMI) Mhe. Suleimani Jafo akijibu maswali ya wabunge
mbalimbali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo
Mjini Dodoma Aprili 19,2017.
Naibu Waziri wa Mambo ya nje ya
Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Susan Kolimba akijibu
maswali ya wabunge mbalimbali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba
wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19,2017.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge
mbalimbali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo
Mjini Dodoma Aprili 19,2017.
Mbunge wa Mwibala (CCM) Mhe.
Kangi Lugola akiuliza swali katika kikao cha tisa cha Mkutano wa saba
wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum Morogoro
(CCM) Mhe. Christina Ishengoma akiuliza swali katika kikao cha tisa
cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akijibu maswali ya wabunge
mbalimbali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo
Mjini Dodoma Aprili 19,2017.
Naibu Waziri wa fedha na Mipango
Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika
kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma
Aprili 19,2017.
Mbunge wa Chilonwa (CCM) Mhe.
Joel Makanyanga akiuliza swali katika kikao cha tisa cha Mkutano wa
saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii Mhe. Ramo Makani akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika
kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma
Aprili 19,2017.
Mbunge wa Viti Maalum Arusha
(CCM) Mhe. Catherine Magige akiuliza swali katika kikao cha tisa cha
Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhe. akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kikao
cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili
19,2017
Mbunge wa Mikumi (CHADEMA) Mhe.
Joseph Haule akiuliza swali katika kikao cha tisa cha Mkutano wa saba
wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Mbunge wa Busokelo (CCM) Mhe.
Fredy Mwakibete akiuliza swali katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba
wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimsikiliza Naibu wake Mhe.
Anastazia Wambura wakati wakijadiliana jambo katika kikao cha Tisa cha
Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakijadiliana jambo na Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Gerson Lwenge katika kikao cha Tisa cha
Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi
Mhe. Charles Tizaba wakijadiliana jambo na Waziri wa Viwanda Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa
saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Wabunge wakifuatilia hoja
mbalimbali katika kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo
Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Picha na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO.
SERIKALI YAFAFANUA JUU YA KUAJIRI
MADAKTARI WALIOKUWA WAENDE NCHINI KENYA, HATUA ILIZOCHUKUA JUU YA
CHANGAMOTO ZITOKANAZO NA AGENDA YA MABADILIKO YA UMOJA WA ULAYA NA
UKARABATI WA NYUMBA ZA NHC NCHINI.
Dodoma, Jumatano, 19 April, 2017.
Serikali imefafanua kuhusu
hatua ilizochukua juu ya kuajiri madaktari waliokuwa waende nchini
kenya, Changamoto zitokanazo na Agenda ya Mabadiliko ya Umoja wa Ulaya
na ukarabati wa nyumba za NHC nchini. Ufafanuzi huo umetolewa leo mjini
hapa.
Madaktari waliotakiwa waende Kenya waajiriwa na Serikali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ameamua kuwa madaktari 258 na wataalamu
wa Afya 11 walioleta maombi na kukidhi vigezo kupitia Wizara ya Afya
kwa ajili ya kwenda kufanya kazi nchini Kenya kuajiriwa na Serikali.
Akifafanua suala hilo Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
amesema makubaliano ya ratiba ya utekelezaji wa ajira hizo za madaktari
hao ilikubalika na pande zote iwe tarehe 6 Aprili 2017 na Madaktari hao
wawe tayari kusafiri kwenda nchini Kenya kati ya tarehe 6-10 Aprili
2017, hadi tarehe ya Taarifa hii Mahakama nchini Kenya haijaondoa
pingamizi lililofunguliwa kuhusu Ajira za madaktari wa Tanzania nchini
Kenya.
Amesema kufuatia uamuzi huu
majina ya Madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa
katika Tovuti ya Wizara pamoja na wataalamu wengine wa afya 11 walioleta
maombi yao na kukidhi vigezo.
Aidha Serikali ya Tanzania
itakuwa tayari kushughulikia upya ombi la Serikali ya Kenya kupatiwa
Madaktari 500, pale ambapo hakutakuwa na vikwazo vya kupeleka madaktari
wetu nchini Kenya.
Mnamo tarehe 18 Machi 2017
Ujumbe wa Serikali ya Kenya ukiongozwa na Waziri wa Afya Dkt.Cleopa
Mailu uliwasili nchini ambapo ulikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli kwa madhumuni ya kuomba kuajiri kwa
Mkataba Madaktari wa Tanzania mia tano(500) ili kupunguza uhaba wa
Madaktari nchini Kenya na kukubali ombi hilo.
Aidha maombi hayo yalipokelewa
ambapo jumla ya maombi 496 yaliwasilishwa na baada ya kufanya uchambuzi
ilibainika kuwa Madaktari 258 walikidhi vigezo vilivyotakiwa kwenda
kufanya kazi nchini Kenya. Lakini wakati Serikali ya Tanzania ikiendelea
kukamilisha utaratibu wa ajira za Madaktari hao Madaktari watano wa
Kenya waliwasilisha pingamizi mahakamani kuitaka Serikali ya nchi yao
kusitisha kuajiri Madaktari kutoka Tanzania.
Changamoto zitokanazo na agenda ya mabadiliko ya Umoja wa Ulaya.
Serikali imesema kuwa
imechukua hatua mahsusi katika kukabiliana na changamoto zinazotokana
na Agenda ya Mabadiliko ya Umoja wa Ulaya.
Akifafanua hoja hiyo, Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Suzan
Kolimba amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali ambazo ni pamoja na
kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kusimamia matumizi ya fedha
za umma ili kuhakikisha tunapunguza utegemezi kwa kiasi kikubwa katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Pia Serikali inaendelea
kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia Sera ya Ubia baina ya Serikali na
Sekta Binafsi ya mwaka 2009 na sheria ya Ubia baina ya Serikali na
Sekta Binafsi ya mwaka 2010. Imebainishwa kuwa mkakati huu unasaidia
kuongeza wigo wa vyanzo za fedha za kugharamia miradi ya maendeleo na
kupunguza utegemezi kwa wahisani.
Hata hivyo Serikali inaendelea
kuwashawishi wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuwekeza zaidi
nchini na zinaenda sambamba na uboreshaji wa mazingira ya kufanyia
biashara nchini na kupunguza gharama za kufanya biashara na uwekezaji
ili kuvutia wawekezaji zaidi kuwekeza nchini.
Katika kuratibu uhamasishaji
wa watanzania waishio ughaibuni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki imeanzisha Idara maalum ya kuratibu masuala ya
Diaspora ili kushiriki katika Maendeleo ya Nchi ikiwemo kuwekeza nchini.
Serikali kuendelea na ukarabati wa nyumba za NHC.
Wizara ya Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imesema kuwa Shirika la Nyumba nchini(NHC)
limeweka mkakati wa kuhakikisha nyumba zote zilizo katika hali ya
uchakavu zinafanyiwa ukarabati mkubwa na zile ambazo kiwango cha
uchakavu ni kikubwa zinavunjwa na kuendeleza upya viwanja hivyo.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula amesema Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) limeshafanya uhakiki wa nyumba zake zote na kubaini hali
halisi ya kila nyumba na kuweka mpango wa kuzifanyia ukarabati nyumba
hizo kwa awamu.
Amebainisha kuwa katika mwaka
wa fedha 2016/17 shirika lilitenga takribani shilingi bilioni 11 kwa
ajili ya kuzifanyia ukarabati nyumba zake ambapo hadi mwezi Machi, 2017
jumla ya nyumba 2451 zilikuwa zimekwishafanyiwa ukarabati kupitia bajeti
hiyo.
Aidha amesema kuwa shirika
hilo linatarajia kumaliza ukarabati wa nyumba zote katika mwaka wa fedha
2017/18 na kusisitiza kuwa matengenezo ya nyumba hizi ni kazi endelevu
kwa shirika hivyo bajeti ya matengenezo itaendelea kutengwa kila mwaka
ili wapangaji wa nyumba za shirika waendelee kuishi katika nyumba na
mazingira bora.
Imetolewa na:
Idara ya Habari-MAELEZO.
No comments:
Post a Comment