Shirikisho Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), linaalika umma kuwania zabuni ya kubuni mwonekano mpya
wa jezi mpya za timu ya taifa zitakazotumika kwa msimu wa 2017/18 na
msimu wa 2018/19.
Kwa taarifa hii, TFF imefungua
milango kwa umma ambako mtu mmoja mmoja anaweza kuwasilisha ubunifu wa
mwonekano wa jezi hizo katika ofisi zake zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo,
Ilala jijini Dar es Salaam.
Wakati mwisho wa kupokea zabuni
hizo ni Novemba 30, 2016, sharti kwa mbunifu ni kutoiga ubunifu kutoka
makampuni makubwa ya vifaa vya michezo. Na Mbunifu Bora au Mshindi wa
jezi ambazo zitakuwa lazima ziwe na nembo ya TFF na Bendera ya Taifa,
atazawadiwa shilingi milioni mbili (Sh milioni 2).
Jezi za sasa za Timu ya Taifa ni rangi ya bluu kwa michezo nyumbani na nyeupe mechi za ugenini.
No comments:
Post a Comment