- CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, kimetakiwa kuona umuhimu wa kuithamini
Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho sambamba na kuwalipa posho makatibu
wake kwani wamekuwa wakitekeleza majukumu yao bila kupewa fedha yoyote,
anaandika Christina Haule.
- Mwajuma
Salim, Katibu wa jumuiya hiyo wilaya ya Morogoro Mjini amesema hayo
wakati akisoma taarifa fupi ya kazi na uhai wa Jumuiya ya Wazazi katika
wilaya hiyo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka 2016.
- Mwajuma
amesoma taarifa hiyo mbele ya Josephat Chacha, katibu wa jumuiya hiyo
Mkoa wa Morogoro ambapo amedai kuwa makatibu hao wanapaswa kupata posho
ili kuongeza morai ya kazi kama makatibu wa chama wanavyopewa.
- “Tunaomba
suala hili la posho lizingatiwe kwani tunafanya kazi kubwa ya kukijenga
chama katika ngazi mbalimbali bila kupewa chochote na pia tunakabiliwa
na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya viongozi wa serikali kukidharau
chama na jumuiya zake jambo linalovunja nguvu ya kufanya kazi,” amesema.
- Awali
Chacha ambaye ni katibu wa jumuiya hiyo mkoa aliwasihi viongozi CCM
kujenga tabia ya kufanya vikao mara kwa mara ili kuhakiki uhai wa chama.
- “Vikao
vina uwezo mkubwa wa kuimarisha chama kufuatia wanachama wengi
kutambulika na kuona umuhimu wa kulipa ada zao kwa wakati jambo
litakalosaidia kuongeza mapato na kuboresha maendeleo ya jumuiya ya
Wazazi,” amesema Chacha.
No comments:
Post a Comment