Sehemu ya kingo za Mto Mkondoo zilizoharibiwa na uharibifu wa mazingira Wilayani Kilosa
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James
Ihunyo (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba katika mkutano na
wananchi katika Kijiji cha Katarukila akiwa ni muendelezo wa ziara yake
ya kikazi katika Mkoa wa Morogoro
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Katurukila na kuwapongeza kwa kuwa Kijiji cha mfano kwa
kuonyesha jitihada za dhati za kuhifadhi mazingira.
Bwana Candidius Songela
akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira January Makamba akingalia ramani inayo onyesha eneo lenye
mgogoro baina ya wanakijiji wa Katarukila na mwekezaji. Katikati ni Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo.
Na Lulu Mussa-Kilombero
Wananchi wa Kijiji cha
Katurulika, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro wameahidiwa Mifuko mia
moja ya saruji ili kukamilisha ujenzi wa zahanati katika tarafa yao
inayohudumia wakazi wa vijiji sita.
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameahidi kutoa
mifuko hiyo ndani ya wiki moja ikiwa ni pongezi kwa Kijiji hicho kwa
kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi mazingira na msitu wa Magombera.
Awali, Bwana Dandidius Songela
alimfamisha Waziri Makamba changamoto wanazokutana nazo katika Kijiji
chao kuwa, ni pamoja na mgogoro baina ya Kijiji cha Katarukila na
mwekezaji anayehodhi sehemu ya eneo la Kijiji na kusababisha uharibifu
wa mazingira. Waziri Makamba aliwasihi wanachi wa Kijiji cha Katarulika
kuwa ni jukumu lao msingi kulinda msitu huo kwa nguvu zao zote na
kubainisha kuwa Hifadhi endelevu ya mazingira ndio mustakabali wa maisha
yao.
Waziri Makamba ameliagiza Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) kumpa
mwekezaji huyo “Restoration Order” kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya
mwaka 2004 kwa kumtaka arejesha mazingira katika hali yake ya asili,
kwakuwa ni eneo tengefu.
kwa upande mwingine Waziri
Makamba amemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilombero Bw. Dennis Londo
kuhakikisha wanasheria wa Manispaa wanahudhuria kesi baina yao na
mwekezaji huyo bila kukosa kila inapotajwa na baada ya kuhumu kutolewa
Waziri Makamba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa
(TAKUKURU) kuchunguza kwa kina endapo kulikua na mianya yoyote ya rushwa
katika mchakato wa kumilikisha ardhi ili kuepuka migogoro ya mara kwa
mara.
Waziri Makamba yuko ziarani Kilombero kuangalia changamoto za mazingira na awali alitembelea Mto Mkondoa Wilayani Kilosa.
No comments:
Post a Comment