Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali akifungua Mkutano wa Majaji
Wafawidhi na Majaji waliosikiliza Kesi za Uchaguzi wa mwaka 2015
unaofanyika jijnini Arusha.
Baadhi ya Waheshimiwa Majaji
Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye Mkutano wa
Kutathmini usikilizwaji wa kesi za uchaguzi unaofanyika jijini Arusha.
Baadhi ya Waheshimiwa Majaji
Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye Mkutano wa
Kutathmini usikilizwaji wa kesi za uchaguzi unaofanyika jijini Arusha.
Na Lydia Churi- Mahakama
Majaji wa Mahakama Kuu nchini
wametakiwa kufanya kazi yao kwa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo
wakati wote kwa kuwa watanzania wanaitegemea Mahakama kuwatendea haki
kwa sawa na kwa wakati.
Akifungua Mkutano wa Majaji
Wafawidhi na Majaji waliosikiliza kesi za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015
unaotathmini usikilizwaji wa kesi hizo leo jijini Arusha, Jaji Kiongozi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali alisema
watanzania wana imani na Mahakama hivyo ni muhimu kwa Majaji hao kutenda
haki wakati wote.
Alisema Majaji hao wamekutana ili
waweze kupata nafasi ya kujadili changamoto mbalimbali zilizojitokeza
wakati wa kusikiliza kesi zilizohusu uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na
kubadilishana mawazo namna ya kuzimaliza kwa haraka kesi zihusuzo
uchaguzi kwa siku za mbeleni.
Alisema jumla ya kesi 53 za
Ubunge zilizotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 zilifunguliwa katika
Mahakama Kuu kanda za Dar es salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya, Moshi,
Mtwara na Mwanza. Kanda nyingine ni Shinyanga, Songea, Sumbawanga, na
Tanga.
Jaji Wambali alisema kati ya kesi
hizo, kesi 31 zilimalizika katika hatua za awali na kesi 22
ziliendelea. Mpaka sasa kesi 19 zimemalizika. Aliongeza kuwa kesi tatu
bado ziko mahakamani.
Jaji Wambali alisema ni jambo la
kujivunia kwa Mahakama ya Tanzania kwa kuwa kesi zote 196 zilizotokana
na uchaguzi wa madiwani zilimalizika mapema katika Mahakama mbalimbali
za Hakimu Mkazi nchini.
Alisema katika kipindi cha mwaka
mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi Mkuu nchini, zaidi ya asilimia 94 ya
kesi za uchaguzi zilizofunguliwa kwenye Mahakama Kuu zimemalizika wakati
asilimia 100 ya kesi zote za udiwani zimemalizika.
Jaji Kiongozi amewapongeza Majaji
na Mahakimu wote kwa kumaliza kesi kwa ufanisi na kwa wakati licha ya
changamoto mbalimbali wanazozipitia Watumishi hao wa Mahakama wakati
wanaposikiliza kesi zainazotokana na uchaguzi.
Aidha Jaji Kiongozi alishukuru
shirika la Umoja wa Mataifa-UNDP kwa kufadhili mafunzo mbalimbali ya
Majaji na Mahakaimu yaliyotolewa kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2015. Mkutano wa siku nne wa Majaji Wafawidhi pamoja na Majaji
waliosikiliza kesi za uchaguzi ulioanza leo jijini Arusha umefadhiliwa
na shirika hilo.
No comments:
Post a Comment