Kamati
ya masaa 72 inatarajia kukaa kujadili vurugu za mashabiki wa Coastal
Union cha kumvamia mwamuzi Thomasi Mkombozi na kumshushia kipigo kama
mwizi baada ya kuwapa penati wageni timu ya KMC ya jijini Dar es salaam.
Ripoti hiyo inajadiliwa baada ya kamishni na FA ya mkoa wa Tanga kuwasilisha ripoti hiyo kwa kamati ya mashindano ya TFF.
Hata
hivyo kumekuwa na hofu kuwa, huenda Coastal Union inaweza kuondolewa
kwenye uwanja huo kutokana na tabia za mashabiki wake kuwapiga waamuzi
mara kwa mara hii ni mara ya tatu walifanya hivyo mwakani kwa kufanya
vurugu dhidi ya Mbeya City Ligi na Yanga FA.
Kwa
upande wa msemaji wa TFF Msemaji, Alfred Lucas, amesema kuwa pamoja na
kusubiria maamuzi ya kamati hiyo, kanuni za wazi ni kwamba iwapo ripoti
zitabainisha mashabiki ndio wenye makosa, basi Coastal kuna hatari ya
kucheza mechi zilizobaki bila mashabiki ama kuhamishwa kutoka uwanjani
hapo.
Mchezo
huo wa Ligi daraja la kwanza ulimalizika kwa Coastal kulala jumla ya
mabao 3-2 na kuendelea kufanya vibaya katika ligi hiyo na ikumbukwe
mwaka jana timu za mkoa wa Tanga ziliweka rekodi Duniani kwa kushuka
zote tatu ambazo ni Coastal,JKT Mgambo na African Sports.
No comments:
Post a Comment