Jokate Mwegelo akiwasili katika
shule ya Sekondari ya Majani Ya Chai ya Vingunguti. Kulia kwake ni Mkuu
wa shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.
Jokate Mwegelo akitoa hotuba yake
katika Mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne ya Shule ya secondari ya
Majani ya Chai. Katika Hotuba yake, Jokate alitoa ahadi ya kuwajengea
uwanja wa michezo na matundu ya Vyoo shuleni hapo. Ujenzi huo utaanza
baadaye.
Mkuu wa Shule ya ya Sekondari ya
Majani ya Chai, Kasango Pascal Ngozi akitoa neno la shukrani baada ya
ahadi ya Jokate Mwegelo wa kujenga uwanja wa michezo na matundu ya vyoo.
Jokate Mwegelo akimkimkabidhi
zawadi ya kuwa mwanamichezo bora wa wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule
ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika mahafali ya nane
ya shule hiyo. Anayeshuhudia (wa kwanza) ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,
Kasango Pascal Ngozi.
Jokate Mwegelo akimkimkabidhi
zawadi mwanafunzi mwenye nidhamu bora kwa kidato cha nne wa Shule ya
Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika mahafali ya nane ya
shule hiyo. Anayeshuhudia (wa kwanza) ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,
Kasango Pascal Ngozi.
Jokate Mwegelo akiserebuka na
wanamuziki wa bongo fleva wanaosoma katika shule ya sekondari ya Majani
ya Chai wakati wa Mahafali ya Nane yaliyofanyika juzi. Jokate ameahidi
kuijengea shule hiyo uwanja wa michezo na matundu ya vyoo.
Na Mwandishi wetu
Mrembo mwenye vipaji lukuki,
Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake yake ya kuchangia jamii ijulikanayo
kwa jina la “Be Kidotified” ameahidi kujenga uwanja wa michezo kwa shule
ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti jijini.
Akizungumza katika Mahafali ya
Nane ya shule hiyo, Jokate alisema kuwa ameguswa na changamoto
mbalimbali zinazo ikabili shule hiyo na kuamua kusaidia kwa kupitia
kampeni yake hiyo.
Tayari Jokate amekabidhi viwanja vya netiboli na mpira wa kikapu kwa shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.
Jokate ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika mahafali hayo, alisema kuwa serikali peke yake haitaweza kutatua
changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu na nyinginezo na hivyo
inahitaji msaada kutoka kwa sekta binafasi na wadau.
“Nashukuru kwa kunichagua kuwa
mgeni rasmi katika mahafali haya, hii imenipa faraja kubwa sana,
nimesikia changamoto mbalimbali, kwa kuanzia nitaanza kujenga uwanja wa
michezo na matundu ya vyoo,” alisema Jokate.
Alisema kuwa ameamua kuonyesha
mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa
kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa
nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na
maendeleo ya elimu hapa nchini.
Mkuu wa Shule hiyo, Kasango
Pascal Ngozi alisema kuwa wanalazimika kutumia viwanja vya shule jirani
katika kufanikisha masuala ya michezo ambayo ni moja ya masomo muhimu
sana.
Ngozi alisema kuwa wanatambua
kuwa kuna vipaji kibao vya michezo katika shule yao, lakini kutokana na
kukosa viwanja bora wameshindwa kuvitambua.
“Tunashukuru Jokate kwa ahadi ya
kutujengea uwanja wa michezo na matundu ya vyoo, hii itatoa hamasa kwa
wanafunzi wenye vipaji katika michezo mbalimbali kutambuliwa na vile
vile kuendelezwa, bado tuna tatizo la jengo la utawala, samani za
ofisini na kumalizia uzio wa shule, tunawaomba wadau watusaidie
kufanikisha hayo,” alisema Kasango.
Mahafali hayo yalipambwa na burudani mbalimbali za muziki wa bongo fleva, singeli, ngoma kutoka kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Kati ya wanafunzi zaidi ya 290
wanaomaliza kidato cha nne, Kkhalid Ibrahim alitwaa tuzo ya mwanamichezo
bora huku Latifa Kihiyo akitwaa tuzo ya mwanafunzi mwenye nidhamu.
No comments:
Post a Comment