Kutoka
kushoto ni Mtafiti Kiongozi wa Afya katika Tume ya Sayansi na
Teknolojia, Dk Khadija Malima na Profesa Henrik Hautop Lund wa Chuo
Kikuu cha Denmark Copenhagen wakikabidhi kifaa maalumu cha mazoezi ya
fiziotherapia utengamao kwa Physiotherapist,
Abdalah Raphael Makala na Kaimu Mkuu wa Idara ya Physiotherapy katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Alex Gomwa.
Mmoja wa watoto wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akifanya mazoezi ya fiziotherapia utengamao leo.
Mmoja wa watoto wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akifanya mazoezi ya fiziotherapia utengamao leo.
Neema Mwangomo, MNH
Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa kifaa maalumu cha kusaidia kuimarisha utendaji wa misuli (training balance and coordination).
Msaada huo umekabidhiwa na Profesa Henrik Hautop Lund kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Denmark Copenhagen.
Profesa Henrik amesema Fiziotherapia Utengamao ni moja ya matibabu ya misuli iliyoathiriwa na magonjwa yaliyoathiri ubongo kutokana na kiharusi au mtindio wa ubongo kutokana na majeruhi wakati wa kuzaliwa.
Profesa
Henrik amekuwa na ushirikiano wa kiutafiti wa utengamao na Dk Khadija
Malima ambaye ni Mtafiti Kiongozi ( Afya) kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia. Utafiti
huo unahusu vifaa (Tiles) vya teknolojia ambayo hutumika kutibu misuli,
mwendo na kuchangamsha akili kwa watoto wenye mtindio wa ubongo wa
kiasi.
“Vifaa
hivi humwezesha mgonjwa kufanya mazoezi na pia kufurahia kama mchezo,
hivyo wateja wanufaika ni wale wenye kiharusi waliopata ajali na
hawawezi kutembea, lakini wanahitaji kuimarisha misuli.
“Lengo
ni kufanya utafiti utakaothibitisha faida ya teknolojia hii ili
kusambaza huduma ya matibabu ya utengamao sehemu zote nchini hata kwenye
jamii kwani teknolojia hii inatumia betri kuchaji na inakaa saa 20,”
amesema Dk Malima.
Pia
teknolojia hiyo imetolewa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa
kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Inuka Rehabilstiona
centre.
No comments:
Post a Comment