Watoto wenye ualbino wapewa mafuta maalum ya kulinda ngozi
Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya na mkurugenzi mtendaji
wa halmashauri ya mji wa Mbinga Robert Mageni waliosimama nyuma wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa chama cha albino wilaya
ya Mbinga, baada ya kukabidhi msaada wa mafuta yenye thamani ya
shilingi laki 8 yaliyotolewa na chama cha walemavu wilayani humo kwa
ufadhili wa hospitali ya KCMC ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma
Robert Mageni,akiteta jambo na mtoto mwenye ualbino ambaye hakufahamika
jina lake mara moja wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mafuta maalum
ya kuzuia magonjwa kwa watu wenye ulamavu wa ngozi yaliyotolewa na
chama cha albino wilaya ya Mbinga.
Sista Judith Mwageni wa shirika la mtakatifu Wiliam jimbo la Mbinga
akiwatambulisha watoto wenye ualbino wanaolelewa na kanisa katoriki
jimbo la Mbinga wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa mafuta maalum ya
kuzuia magonjwa ya ngozi yaliyotolewa na chama cha walemavu wilaya ya
Mbinga.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Robert Magenj
akizungumza jana katika hafla ya kukabidhi mafuta maalum kwa watu wenye
ualbino yaliyotolewa na chama cha walemavu wilaya ya Mbinga kwa ufadhili
wa hospitali ya KCMC ya Moshi,katikati ni katibu tawala wa wilaya ya
Mbinga Gilbert Simya.
Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya akitoa mafuta maalum ya
kuzuia magonjwa kwa watu wenye ualbino jana wakati wa kukabidhi msaada
wa mafuta wenye thamani ya shlingi laki 8 yaliyotolewa na chama cha
walemavu wilayani humo.Picha na Muhidin Amri.
No comments:
Post a Comment