Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Jerry Sabi, bodi imeamua kufungua ofisi zao ili kutoa nafasi kwa wanaohitaji huduma na pia kwa wadaiwa kwenda kutoa malalamiko yao.
Sabi alisema ofisi hizo zitakuwa wazi kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri kwa siku hizo mbili na kuwasisitiza wadaiwa wote wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kulipa watumie fursa hiyo kwenda kufahamu madeni yao.
Katika hatua nyingine, Sabi alisema bodi hiyo itaanza kuwachukulia hatua za kisheria wadaiwa wote ambao hawajaanza kulipa madeni yao, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani, kutozwa faini, kunyimwa fursa za mikopo, masomo nje ya nchi na kuzuiwa kusafiri nje.
No comments:
Post a Comment