Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Dodoma katika
Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa
mjini Dodoma na kutoa tamko la yeye kuhamia Dodoma ifikapo mwezi wa
tisa ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli
kuhamishia serikali makao makuu ya nchi mkoani Dodoma
Baadhi
ya viongozi waliohudhuria maadhimisho hayo wakifuatilia hotuba ya
Waziri Mkuu wakati alipokuwa akiwasalimia wakazi wa Dodoma waliohudhuria
maadhimisho hayo kutoka kushoto ni Naibu Spika Tulia Akson, Spika wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Mohammed Said Mohammed Dimwa, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Meya wa mji Manispaa ya Dodoma Mh. Emmnuel Mwiliko.
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu
kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa
wananchi.
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.
“Jana
nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe
matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma
ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa
Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo.
Amesema tangu
Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na
wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa
ahadi alizotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.
John Magufuli.
“Wananchi kazi
mmeziona na sasa tunaenda kwenye utekelezaji. Ninatoa agizo kuwa
mawaziri na manaibu wote wahame mara moja kutoka Dar es Salaam na kuja
Dodoma. Wana ofisi ndogo Dodoma na kwa kuwa wamekuwa wakiishi wakati
wote wa Bunge, wahamie mara moja. Mimi nahamia Septemba, na utekelezaji
wake nitausimamia kwa juhudi zote,” alisisitiza.
Amewataka
wakazi wa Dodoma watumie fursa hiyo kutunza amani ya nchi na kudumisha
umoja uliopo na pia akataka watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi
za kutosha, nyumba za kulala wageni na hoteli za kitalii ili watu
watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi.
Wakati huo huo,
mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. John Magufuli katika muda wa siku tatu amerudia kusisitiza
nia ya Serikali kuhamia Dodoma katika kipindi chake cha uongozi ili
kutekeleza ndoto ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ya kutaka makao makuu ya nchi yawe Dodoma.
Akizungumza na
mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma kwenye uwanja wa mashujaa huku
akishangiliwa, Rais Magufuli amesema atahakikisha Dodoma inakuwa makao
makuu ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobakia kwenye awamu ya
kwnza ya uongozi wake.
“Kama wabunge
karibu 300 na mawaziri na manaibu wao ambao hawafiki 30 wanakaa hapa kwa
miezi mitatu na maisha yanakwenda, kama makao makuu ya chama
kinachotawala nchi yako hapa sioni sababu ni kwa nini Serikali
ninayoiongoza iendelee kubakia Dar es Salaam,” amesema.
Mara kwanza
kutoa kauli hiyo, ilikuwa ni Jumamosi iliyopita, Julai 23, 2016 wakati
akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkutano Mkuu maalum wa chama hicho.
Rais Magufuli
amesisitiza wananchi na wanasiasa kutunza amani na kudumisha amani
iliyokuwepo nchini. Pia amewataka Watanzania wote kuendelea kuwaenzi
mashujaa walioipigania nchi hii.
No comments:
Post a Comment