Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu KATOKE ( TTC ) kilichopo Kagera Wilaya ya
Muleba walalamika juu ya adhabu wanazopewa na uongozi wa hapo Chuoni
pindi wanapofanya makosa..
Mwanafunzi akieleza hali ya Shuleni hapo..
Mnamo tarehe 27/07/2016 saa 3:28Pm kengele iligongwa kwa ajili ya kwenda
paredi ambapo huwa ni siku ya (EK) Yaan elimu ya kujitegemea ambapo
huwa tunatakiwa kwenda paredi kwa ajili ya kugawiwa majukumu ya kazi.
Kengele inapaswa igongwe saa 3:30pm au saa 4:00pm inategemeana na ratiba
ya siku ila inayofahamika ni saa 4:00pm kwa siku ya jumatano.
Tulichelewa dakika 1 tu paredi basi ikawa ni kosa na ndipo ikasababisha
tukapewa adhabu kama zifuatazo:- 1 kuandika barua kwanini tumechelewa
paredi. 2 tukapewa fomu ya mashitaka, ambapo fomu hii huwa mpaka kamati
ya Nidhamu ijadili na ndipo itolewe tena kwa kosa kubwa aidha
umesimamishwa masomo ila sisi tulipewa fomu ya mashitaka bila hata
kamati ya nidhamu kukaa. 3 Tukapewa adhabu ya kung'oa GOGO ambalo mtii
ulipandwa miaka mingi sana iliyopita pindi chuo kipo kwa matumizi ya
kikoloni na hayo magogo au visiki mizizi yake kwa ukubwa unapasua mbao. 4
mwalimu aliyetupa adhabu kawatoa baadhi ya wasichana katika adhabu. 5
Aliahidi atatuandika katika black book.
Kwa mjibu kosa haliendani na adhabu aliyotoa kwani hata tungeandika
barua ilikuwa ni adhabu tosha. katika adhabu tulikuwa 30 ila kwa sasa
tuko 23 ambapo kila kisiki kina watu 8 na wengine wanafyeka msitu mnene
kweli. Binafisi sisi tumechukizwa sana pia rais wa chuo hana sauti. Hivi
visiki hata tukichimba mwezi labda ndio vitakamilika ila module
zitakuwa zimetupita na usomaji utakuwa wa taabu. Tunaomba mtusaidie ili
haki itendeke pia kuna MICHANGO YA KIHOLELA WANATUCHANGISHA HALAFU
HATUELEWI MANUFAA YAKE MANA TUKIHOJI HAWASEMI WAZI. CHUO CHA UALIMU
KATOKE-BUKOBA.
No comments:
Post a Comment