Wednesday, 27 July 2016

Viboko watishia maisha ya wakulima wa Malinyi

Morogoro. Wakulima wa Kijiji cha Ihohanja Kata ya Kilosa kwa Mpepo, wilayani Malinyi wanahofia maisha yao baada ya viboko kuvamia mashamba yao.
Diwani wa Kilosa kwa Mpepo, Boniventure Kiwanga amesema viboko hao wamekuwa tishio kwa wakazi wa kata hiyo.

Amesema wanyama hao wamevamia mashamba ya mahindi karibu yote.

Amesema wakulima hao ambao hulima zaidi zao la mpunga, safari hii wamelazimika kupanda mahindi baada ya mpunga kusombwa na mafuriko ya mvua za masika zilizonyesha msimu huu.

“Lakini viboko nao wanawapa shida, wengi wameingiwa na hofu ya kukumbwa na baa la njaa,” amesema diwani huyo.

No comments:

Post a Comment