Utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kufanya usafi wa mazingira kila siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi limeanza kukiukwa na baadhi ya wananchi kutokana na idadi ndogo ya watu ambao imejitokeza mwezi huu kufanya usafi mitaani, hali ambayo imesababisha baadhi ya wananchi kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya yanaokiuka agizo hilo.
Akizungumzia suala hilo, mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Nachoa Zakaria amekiri baadhi ya wananchi hasa wafanyabiashara kutojitokeza kufanya usafi kama ilivyopangwa na akaahidi kutumia sheria ndogo za jiji kuwashughulikia.
Mkuu wa wilaya ya mbeya, Paulo William ntinika ambaye pia ameingia mitaani kufanya usafi, ametoa wito kwa wananchi kujenga mazoea ya kujitokeza kufanya usafi wa mazingira ili maeneo yao ya biashara na makazi yaweze kuwa safi.
No comments:
Post a Comment