Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana
na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea leo
jijini Dar es Salaam na Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na
Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa
kuhamia Dodoma, Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye Ulemavu), Dr. Abdallah Possi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana
na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea leo
jijini Dar es Salaam na Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na
Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu utekelezaji wa
kuhamia Dodoma, Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Watu wenye Ulemavu), Dr. Abdallah Possi.
Baadhi
ya Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya
Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Jenista Mhagama wakati wa
kikao kuhusu utekelezaji wa kuhamia Dodoma.
Na Jonas Kamaleki, MAELEZO
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Uratibu,Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu itahamia Dodoma juma
lijalo kufuatia agizo la Mhe. Rais John Pombe Magufuli la Serikali
kuhamia Dodoma.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi ,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati
akiongea na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizoko chini
ya ofisi hiyo.
“Mchakato wa kuhamia Dodoma
umekwisha kilichobaki kwa sasa ni utekelezaji, mimi na manaibu mawaziri
wangu tunahamia juma lijalo ili tukamkaribishe Mhe. Waziri Mkuu
anayehamia Septemba mwaka huu,” alisema Mhagama.
Mhagama amesema kuwa kila
kiongozi anayehamia Dodoma inabidi awakute walio chini yake tayari
wamekwishahamia ili kumpokea, hivyo akawataka na watendaji ambao wako
chini yake watangulie kwa ajili ya kumpokea yeye na viongozi wenzake.
Aidha, Waziri huyo amesema kwa sasa hakuna mjadala wa kuhamia Dodoma lilobaki ni utekelezaji tu wa kuhamia Makao Makuu.
Mhagama amesema kama kuna Taasisi
chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imetenga fedha kwenye bajeti kwa ajili ya
ujenzi, shughuli hiyo ikafanyike Dodoma ambako Serikali inahamia. Kwa
kusema hivyo kadhalika na ofisi au Wizara nyingine za serikali ambazo
zimetenga fedha ya ujenzi wakajenge Dodoma.
Suala la kuhamia Dodoma sio geni
bali limekewepo kwa kipindi kirefu ila utekelzaji wake ndio ulikuwa
bado; pia katika Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 suala hili lipo,
alisema Mhagama na kuongeza kuwa kipindi cha nyuma Wizara saba (7)
ziliwahi kuhamia Dodoma na kwa sasa Wizara inayoshughulikia Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iko Dodoma.
Waziri Mhagama ameipongeza Tume
ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuanza ujenzi wa jengo lake mjini Dodoma na
kusisitiza kuwa Wizara na Taasisi nyingine za Serikali kuiga mfano huo
kwa kujenga ofisi zao Dodoma.
“Kwa kuwa sisi ni waratibu wa
wizara zote inabidi tuunde kikosi kazi kitakachofanya kazi ya uratibu wa
kuhama kikiwa Dodoma ili kuwawezesha na watumishi wenzetu kutekeleza
agizo la Mhe. Rais la serikali nzima kuhamia huko,”alisema Mhagama.
Mhagama amesema kuwa Mamlaka ya
Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA) wameshafanya kazi nzuri ya
upimaji eneo la serikali ambalo litatumika kwa ajili ya ofisi.
“Tumefika mwisho wa mchakato sasa
ni utekelezaji na tunataka watumishi walielewe vizuri suala hili na
wawe tayari kulipokea,”alisisitiza Mhagama.
Kuhamia Dodoma katika kipindi
hiki kunatokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alillolitoa tarehe 27 Julai, 2016 mjini
Dodoma kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambo ulimchagua kuwa Mwenyekiti
wa tano wa chama hicho tawala.
No comments:
Post a Comment