Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Utangazaji la Japan NHK, mtuhumiwa wa shambulio hilo anashikiliwa na Jeshi la polisi la nchini humo.
Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 26, alikamatwa na Polisi akiwa katika jaribio la kujiua.
Vituo kadhaa vya televisheni nchini Japani vimekuwa vikionyesha idadi kubwa ya magari ya wagonjwa yakibeba wagonjwa kutoka kwenye eneo la tukio na kuwakimbiza kwenye hospitali ya jirani.
Taarifa za awali zilizotolewa na Shirika la habari la Kyodo zilieleza kuwa watu 19 walifariki na 20 kujeruhiwa taarifa ambayo baadaye ilisahihishwa.
No comments:
Post a Comment