Wakati tukiendelea kutafakari juu makaburi hayo fahamu kuwa hata katika nyumba za ibaada huko ughaibuni mambo yameanza kwenda kidigitali.
Hii ni baada ya MMkanisa ya Kiprotestanti nchini Ujerumani kuazimia kutoa fursa kwa waumini wake kuingia katika mtandao kwa kuwawekewa huduma ya Wi-fi bila malipo.
Huduma hiyo itapatikana katika maeneo mbayo, kwa kufuata ‘hostpots’ ambalo ni jina la vitovu vya huduma yamepewa jina “Godspots,”.
Huduma hiyo itawekwa katika makanisa 220 ikihushisha majimbo ya Berlin na Brandenberg. Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha RBB, mpango huo baadaye utatekelezwa katika makanisa 3,000.
Makanisa ya kwanza kupata huduma hiyo yatakuwa kanisa kuu la French Cathedral eneo la Gendarmenmarkt na kanisa la Kaiser Wilhelm Memorial. Watu wataweza kutumia huduma hiyo kutoka ndani na nje ya kanisa.
Wanaotumia huduma hiyo watatakiwa kuwa na ukurasa wa tovuti yenye maelezo kuhusu kanisa lenyewe, jamii na maelezo ya kidini. Lakini baadaye wataweza kutafuta chochote watakacho katika mtandao wote.
Huenda huduma hii ikiingia Tanzania makanisa mengi yatajaa kwani kwa siku za hivi karibuni watumishi wa Mungu wamekuwa wakihubiri juu ya mahudhurio hafifu.
No comments:
Post a Comment