Mkaguzi wa viuatilifu kutoka makao makuu ya taasisi ya viuatilifu, TPRI,jijini Arusha,Godfather Kaguo,ndiye ambaye ameendesha zoezi la ukaguzi kwenye maduka ya pembejeo za kilimo jijini Mbeya na kufanikiwa kukamata shehena ya viutalifu ambavyo havijasajiliwa nchini vikiwa vimesheheni madukani.
Peter Lusokana ni Mkaguzi wa viuatilifu kanda ya nyanda za juu Kusini ambaye amesema kuwa kuna madhara makubwa ya matumizi ya viuatilifu ambavyo havijasajiliwa nchini,ikiwemo uharibifu wa mazingira,athari za kiafya kwa watumiaji pamoja na kutokuwa na uhakika wa ubora wake.
Baadhi ya wauzaji na wamiliki wa maduka ya pembejeo za kilimo wamesema kuwa baadhi ya viuatilifu hivyo huvinunua nchi jirani kutokana na kuuzwa kwa bei chee,huku wakiwa hawana elimu ya kutambua viuatilivyo ambavyo havijasajiliwa.
No comments:
Post a Comment