Hawa ndo mahasimu katika vilabu vyao
10. PJANIC & DZEKO, Bosnia
Wawili hao ni wachezaji wa timu ya taifa ya Bosnia walikuwa pamoja
kwenye kikosi cha Roma hadi pale Pjanic alipohamia Juventus hivi
karibuni.
Dzeko na Pjanic walikuwa ni msaada mkubwa ndani ya Roma, lakini kuanzia
msimu huu watacheza wakiwa wapinzani kutokana na Pjanic kujiunga na
‘kibibi kizee cha Turin’ huku Dzeko akiendelea kusalia Roma.
9. ZABALETA & ROJO, Argentina
Pablo Zabaleta amekuwa akiitumika Man City tangu mwaka 2008 na amefanya
kazi nzuri hadi sasa. Rojo alijiunga na United misimu miwili iliyipita
lakini bado hajaonesha uwezo mkubwa kuwashawishi mashabiki wa ‘Mashetani
wekundu’.
8. MARTIAL & GIROUD, France
Martial alijiunga na Manchester United msimu uliopita na kwa haraka
akafunga magoli muhimu kwa timu yake, huku Olivier Giroud akiwa ndiye
mshambuliaji muhimu kwa Arsenal kw sasa.
7. KEVIN DE BRUYNE & FELLAINI, Belgium
De Bruyne na Fellainini wachezaji kutoka vilabu viwili hasimu zaidi vya
jijini Manchester ambao wanaheza pamoja kwenye timu taifa. De Bruyne
akiwa Manchester United wakati Fellainini yeye anaitumikia klabu ya
Manchester United.
6. PISZCZEK & LEWANDOWSKI, Poland
Wa
poland hawa wawili walikuwa pamoja pia kwenye klabu ya Borussia
Dortmund kabla ya Lewandowski kuamua kuihama klabu hiyo na kuhamia
Bayern Munich.
5. MODRIC & RAKITIC, Croatia
Hawani viungo mafundi wa timu ya taifa ya Crpatia ambao hukutana kwenye
pambano la El Clasico linalovihusisha vilabu viwili hasimu zaidi katika
historia ya soka la Hispania. Modric akiwa upande wa Real Madrid wakati
Rakitic anaiwakilisha Barcelona.
4. ROONEY & STURRIDGE, England
Watoto hawa wa taifa la England wamekuwa na mchango mkubwa kwenye safu
ya ushambuliaji ya timu yao ya taifa kwa miaka kadhaa sasa.
Lakini inapofikia kwenye ngazi ya vilabu, wawili hawa wanageuka na kuwa
maadui wakubwa linapopigwa pambano linalozihusisha Liverpool
anayoichezea Sturridge dhidi ya Manchester United inayowakilishwa na
Rooney.
3. SCHWEINSTEIGER & OZIL, Germany
Bastian alisaini kujiunga na Manchester United msimu uliopita na
kukutana na mjerumani mwenzake Ozil anayekipiga England kwenye klabu ya
Arsenal. Bastian amerejea kutoka majeruhi wakati Ozil ni mchezaji muhimu
kwa upande wa Arsenal, itavutia san kushuhudia namna ya wajerumanin
hawa watakavyofanya pale klabu zao zitakapokutana msimu huu.
2. MARCELO & NEYMAR, Brazil
Real Madrid v FC Barcelona ni game yenye upinzani mkubwa sana kwenye
ligi ya Hispania si tu kwasababu vilabu hivi vinamajina makubwa nchini
humo, bali pia ni kutokana na vikosi vya timu hizi kuundwa na wachezaji
wenye uwezo wa hali ya juu na wenye majina makubwa kwenye ulimwengu wa
soka.
Marcelo akiwa Real Madrid na Neymar akiwa Barcelona, wote wanacheza timu
ya taifa ya Brazil lakini inapofika katika ngazi ya klabu kila mmoja
anapambana kuhakikisha timu yake inapata ushindi na kuibuka na vikombe
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment