Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina ( katikati) Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Khatib Kizinga
(kushoto) wakipata maelezo toka kwa Bw. Sultani Pwaga wa kiwanda cha Gas
cha Madiba Mjini Mtwara wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mpina kiwandani
hapo.
Serikali imekitoza faini ya shilingi milioni 15, kiwanda cha
kutengeneza simenti cha Dagonte Industry Limited kilichopo mjini Mtwara,
kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira
Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
NEMC limekitoza faini ya shilingi milioni 15, kiwanda cha kutengeneza
simenti cha Dagonte Industry Limited kilichopo mjini Mtwara, kwa kosa la
kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.Katika siku ya pili ya ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina mkoani Mtwara imebainika kuwa kiwanda hicho cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu tangu kianze kazi ya kutengenza simenti, kimefanya uchafuzi wa mazingira kwa kukosa sehemu maalum ya kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani hapo.
Mkosa mengine ni kukosa vyoo kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva na makondakta wanao chukua mzigo wa simenti kiwandani hapo, na kusafirisha kwenda sehemu mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafisha sehemu ya nje ya kiwanda hicho ambapo imeelezwa kuwa eneo hilo la nje wakati wa kipindi cha mvua mazingira yake huatarisha afya ya watumiaji wa eneo hilo.
Kwa Mujibu wa Naibu Waziri Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili, inaenda sambamba na urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani hapo pamoja na kuamsha uongozi wa kiwanda hicho kwa kudharau sheria ya mazingira, na kutaka kiwanda hicho kuajiri afisa mazingira atakayeshughulia changamoto hizo.
Kwa upande wake meneja utumishi na utawala wa kiwanda hicho Bw. James Kajeli aliomba serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa kwenye mpango wa kufanya marekebisho hayo na kuongeza kuwa kutokufanya hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa baadhi ya miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na upatikani wa baadhi ya vibali kutoka katika taasisi za serikali na si kudharau sheria ya mazingira.
Naibu Waziri Mpina pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza gas cha Madiba na kukisifu kwa utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa viwanda vya serikali, kuwa mfano katika kutii sheria za mazingira.
Ziara ya Mhe. Mpina pia ilihisisha ukaguzi wa kiwanda cha kubangua korosho cha micro mix cha mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha Solvochemi pamoja na fukwe ya mnazi bay iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
No comments:
Post a Comment