Kuondoka kwa Uingereza kutoka EU kumeathiri uchumi duniani
Mkutano wa mawaziri wa fedha wa mataifa ya G20, umemalizika nchini
China, huku onyo likitolewa kuwa, kura ya maoni iliyoifanya Uingereza
kujiondoa ndani ya muungano wa mataifa ya Bara Ulaya, imesababisha
hatari kubwa zaidi na kuyumbisha uchumi wa Dunia.
Mkutano huo wa G20 umesema kwamba kuna hatari kubwa kuwa, mazungumzo
kuhusiana na hatua hiyo ya Uingereza yakaibua uchungu mwingi.
Lakini viongozi hao wakasema kuwa EU imejiandaa ipasavyo kushughulikia
tatizo hilo huku wakisema kuwa wana matumaini kubwa kuwa Uingereza
sharti iendelee kuwa mshirikamkubwa wa EU.
No comments:
Post a Comment