Friday, 29 July 2016
Mo kutoa Sh bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 na kuwekeza ndani ya Simba.
Mfanyabiashara kijana na mwenye mafanikio makubwa nchini, Mohammed Dewji amesema angependa kuwekeza Simba ili kubadili mfumo.
Dewji maarufu kama “MO”, amewaambia waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo jijini DAr es Salaam kwamba bajeti ya Yanga na ile ya Azam FC ni mara mbili ya ile ya Simba, jambo linaloifanya klabu hiyo kuendelea kubaki kuwa msindikizaji.
Tayari Mo amesema yuko tayari kutoa Sh bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 na kuwekeza ndani ya Simba.
“Kama unataka mafanikio kwenye mpira, hakuna zaidi ya fedha. Simba haiwezi kuwa na miaka 80 leo haina hata uwanja wa mazoezi.
“Unajua kama nikiwekeza fedha hizo, tunaweza kuzipeleka kwenye mkopo na kuikopesha serikali. Baada ya hapo tutapata faida ya dola bilioni 7.5 ambazo tutaziingiza kwenye maendeleo.
“Mimi ninaamini Simba haiwezi kubadilika kwa kuwekeza kwenye bajeti ya Sh milioni 500 kwa mwaka. Haitawezekana, ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza, kwanza Simba inahitaji muwekezaji na si mdhamini.
“Nisisitize hili,mimi ni mwanachama wa Simba, ninaumia kuona timu hii inakwenda hivi. Ndiyo maana ninaingia nikiamini nitaweza kubadilisha mambo kwa kushirikiana na wanachama wa Simba ili kuleta mabadiliko katika klabu ye
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment