Nafasi ya Yanga nusu fainal ya CAF imezidi kuwa finyu baada ya kipigo 3 - 1
July 26 2016 ilikuwa ni siku nyingine kwa wawakilishi pekee wa Tanzania
katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika, klabu ya Dar es
Salaam Young Africans kucheza mchezo wake wa nne wa Kundi A Kombe la
shirikisho barani Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana.
Yanga wamecheza mchezo wao wa nne dhidi ya Medeama mjini Takoradi Ghana
na kukubali kipigo cha goli 3-1, kipigo ambacho kimezidi kufifisha
safari ya Yanga kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo,
magoli ya Medeama yamefugwa na Daniel Amoah dakika ya 7 na Abbas
Mohammed aliyefunga magoli mawili dakika ya 22 na 37.
Simon Msuva ndio aliyefunga goli la kufutia machozi kwa Yanga kwa mkwaju
wa penati dakika ya 24, kwa matokeo hayo Yanga wanaendelea kusalia na
michezo miwili dhidi ya MO Bejaia ya Algeria watakaocheza nyumbani na TP
Mazembe ya Kongo watakaocheza ugenini, nafasi ya Yanga kufuzu katika
hatua ya nusu fainali ni finyu sana.
No comments:
Post a Comment