IGP Mangu akagua miundombinu ya kipolisi mkoani Shinyanga
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, akiwa katika ziara ya
kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi katika wilaya ya Kishapu
Mkoani Shinyanga jana, kulia ni kamanda wa Polisi mkoani humo, Muliro J.
Muliro.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akifuatilia jambo
kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Mhe. Fadhil Nkhulu
(aliyesimama) anayefuata ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab R.
Telack, pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo
wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akifafanua jambo
wakati alipomtembelea ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Msalala mkoani Shinyanga, Mhe. Simon S. Berege (katikati), akiwa
katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi, kulia ni
kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Muliro J. Muliro.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akiangalia kwa umakini
ramani ya mipango miji inayoonesha mahala itakapokuwepo Makao Makuu ya
Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga, katikati (aliyevaa tai) ni
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Msalala Mhe. Simon S. Berege,
wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi
katika mkoa wa Shinyanga.
No comments:
Post a Comment