Tuesday, 26 July 2016

Watumishi 8 wasimamishwa kazi wilayani Gairo

Watumishi nane wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro wamesimamishwa Kazi Kupisha uchunguzi wa Tuhuma za ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Akizungumza katika ofisi za Halmashauri ya wilĂ ya ya Gairo,Mkurugenzi mpya wa halmashauri hiyo,Agnes Mkandya amesema uamuzi wa kuwasimamisha watumishi hao ulifikiwa na ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro,kufuatia tume maalum iliyoundwa kuchunguza tuhuma katika halmashauri hiyo,kwa maelekezo ya Waziri wa Tamisemi baada ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha.


Barua za kusimamishwa kazi kwa watumishi hao zilitumwa kwa mkurugenzi wa awali wa Gairo Mbwana Magotta,(aliyeachwa kwenye uteuzi) na katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk John Ndunguru,ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kuundwa kwa tume hiyo maalum na mkuu wa Mkoa wa Morogoro  ili kuchunguza madai mbalimbali ya madiwani wa wilaya hiyo,ikiwa ni maelekezo ya waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na maelekezo hayo kuwasilishwa kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro na Katibu mkuu Wizara ya Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Tamisemi,Musa Ibrahim Iyombwe.

Watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni kutoka idara za Afya, Elimu, Mipango na Fedha ambao ni Tumaini Njeleka, Godlover Nnko,Josephat Lyombo,Rajabu Mushi,Mustafa Kachelele,Willy Chiwaye,Edward Mkumbo na Karimu Sululu ambaye anaruhusiwa kughushi hundi ya zaidi ya shilingi milioni 15.

Mkurugenzi huyo mpya wa Gairo amewataka watumishi katika halmashauri hiyo kufanya kazi kwa weledi,uadilifu na uaminifu na kuacha kutumia fedha za miradi ya maendeleo inayopitia katika idara zao ovyo na tofauti na maelekezo ya Serikali huku akionya kutofumbia macho hali hiyo na mianya yeyote ya matumizi mabaya ya fedha.

No comments:

Post a Comment