Thursday, 28 July 2016

Magazeti 45 na vituo 16 vya Luninga nchini Uturuki vimefungiwa

Mamlaka nchini Uturuki imevifungia kufanya kazi vyombo kadhaa ya habari nchini humo, kufuatia jaribio la Mapinduzi lililoshindwa.
Magazeti 45 na vituo 16 vya Luninga vimeamriwa kufungwa kwa tuhuma za kuchochea uasi huo.
Tayari mamia ya watu wamewekwa kizuizini kwa kuhusisha na jaribio hilo la mapinduzi.

Viongozi wa upinzani kutoka vyama vya Republican na Nationalist wameelezea kuunga mkono hatua hiyo ya serikali.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewataka maafisa wa Uturuki, kupeleka ushahidi haraka ili mahakama ziweze kutoa maamuzi ya kisheria haraka kwa watuhumiwa hao.

No comments:

Post a Comment