Manchester City 6-5 Borussia Dortmund
Mkufunzi mpya wa Manchester City,Pep Guardiola, amesajili ushindi wake
wa kwanza tangu atue Manchester City baada ya kuwaongoza mabingwa hao wa
zamani wa ligi kuu ya Uingereza kuwalaza Borussia Dortmund katika
kinyang'anyiro cha kutafuta mabingwa wa vilabu vya kimataifa huko China.
Kipa chipukizi wa Man City Angus Gunn, 20, aliokoa mkwaju wa penalti wa
Mikel Morino na kuwahakikishia vijana wa Pep ushindi wa mabao 6-5.
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Longgang ulioko Shenzhen ilikuwa imeishia sare ya 1-1 katika muda wa kawaida.
Sergio Aguero alikuwa ameiweka Man City kifua mbele mapema katika mechi
hiyo lakini mshambulizi chipukizi wa Dortmund Christian Pulisic, mwenye
umri wa miaka 17, kuwasawazishia wajerumani hao katika muda wa majeruhi.
Hii ndio ilikuwa mechi ya kwanza kwa Man City baada ya mechi iliyokuwa
imepangwa awali dhidi ya vibonde wao wa jadi kutoka Uingereza Manchester
United kuahirishwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mjini Beijing.
No comments:
Post a Comment