Alisajiliwa na Juventus akitokea klabu ya Manchester United mwaka 2012 baada ya kumaliza mkataba wake na klabu hiyo. Sasa amekuwa mchezaji wa kiwango cha juu ulimwenguni baada ya kutoa mchango mkubwa kwa Juve kutwaa taji la Serie A mara nne mfululizo.
Endapo dili hilo litawafanikiwa basi Pogba atakuwa ameungana na wachezaji hawa ambao awali waliondoka klabu zao na kurejeshwa kwa donge nono.
7. Marco Reus – Borussia Dortmund
Baada ya Borussia Monchengladbach wakamsajili kutokea hapo kabla Dortmund kumrejesha tena kwa ada ya paundi mil 14.5 mwaka 2012.
6. Peter Crouch – Tottenham Hotspur
Crouch
ni zao la miamba hiyo ya White Hart Lane lakini aliuzwa kwa Queens Park
Rangers mwaka 2000 kwa ada ya paundi 60,000. Baadaye alirudi tena mwaka
2009 kwa ada ya paundi mil 10.
5. Nicolas Anelka – Paris Saint Germain
Baadaye Mfaransa huyo alihamia tena Real Madrid kabla PSG hawajamrudisha mwaka 2002 kwa ada ya paundi mil 22.
4. Mats Hummels – Bayern Munich
Mapema kwenye usajili wa kiangazi msimu huu, Munich waliamua kumrejesha kwa ada ya paundi mil. 28.
3. Nemanja Matic – Chelsea
Akiwa Benfica alicheza vizuri na mwaka 2014 Chelsea kuamua kumrejesha kwa ada ya paundi mil 21.
2. Paul Pogba – Manchester United
1. Cesc Fàbregas – Barcelona
Mwaka 2011, Fàbregas alirejea tena Barcelona kwa ada ya paundi mil 35 baada ya kuichezea Arsenal zaidi ya michezo 300.
No comments:
Post a Comment