Abiria wakiwa wamepanda kwenye Kirikuu.
Abiria wakitafuta usafiri.
Wengine wakipanda kwenye pikipiki ya magurudumu matatu.
Madereva wakiwa kwenye mkusanyiko.
Askari polisi wakiwa eneo la tukio, Nyegezi Kona.
Taharuki eneo la tukio.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya madereva daladaa waliokuwa wamekusanyika na kugoma kusafirisha abiria mkoani humo.
Tukio hilo limetokea mapema leo jijini humo wakati madereva hao walipogoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria kwa madai kuwa wamekuwa wakitozwa kodi na faini za mara kwa mara bila kuzingatia sheria na kanuni za makosa ya barabarani.
Akizungumza na mwandishi wetu aliyeko jijini Mwanza, mmoja wa madereva hao waliokuwa wamekusanyika kwenye Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani cha Nyegezi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema wamechoshwa na vitendo vya askari wa usalama barabarani kuwatozwa kodi kila mara bila kuzingatia sheria wakati na wao (madereva) kipato chao kinategemea kazi hiyo.
Madereva hao wamezitaka mamlaka husika ziliangalie suala hilo kwa jicho la tatu ili waweze kufanya kazi zao kwa amani na uhuru bila manyanyaso.
Mbali na adha ya kupigwa mabomu ya machozi, mpaka saa 6 mchana, abiria walikuwa bado wapo vituoni wakihangaika kutafuta usafiri wa kuwapeleka kwenye shughuli zao huku wengine wakilazimika kutumia usafiri usio rasmi kwa kubanana kwenye gari aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Virikuu’ na pikipiki za mizigo za magurudumu matatu.
No comments:
Post a Comment