Thursday, 21 July 2016

Urusi hawatashiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka huu


 
Wanariadha wa Urusi hawatashiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka huu huko Brazil.
kauli hiyo imeafikiwa na mahakama ya juu ya michezo ambayo imefutilia mbali rufaa
iliyowasilishwa na kamati ya olimpiki ya Urusi ROC ya kuitaka ibatilishe uamuzi wa shirikisho la riadha duniani IAAF wa kuwapiga marufuku wanariadha wake wote wasishiriki michezo ya olimpiki itakayoandaliwa jijini Rio De Jenairo Brazil kuanzia mwezi ujao.


IOC inatathmini hatua za kisheria dhidi ya Urusi

Urusi ilitoa dawa zilizopigwa marufuku kwa wanariadha wake ,Ripoti

IAAF ilifikia uamuzi huo baada ya ufichuzi kuwa serikali ya Urusi ilikuwa na mpango wa chini kwa chini wa kuficha matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku miongoni mwa wanariadha wake.

Olimpiki: Urusi kujua hatma yao Julai 21

Kamati ya olimpiki ya Urusi ilikuwa imekata rufaa kwa pamoja na takriban wanariadha 68 ambao hawajawahi kupatikana na hatia ya matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.

IOC inatathmini hatua za kisheria dhidi ya Urusi

Baada ya kusikiza pande zote mbili mahakama hiyo ya juu katika riadha CAS imeamua kufutilia mbali rufaa hiyo.

Kauli hiyo imewadia siku moja tu baada ya uchunguzi huru kubaini kuwa wizara ya michezo ya Urusi, na kamati ya kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini ya Urusi zilishiriki udanganyifu ikiwemo kubadilisha mikojo ya wanariadha ilivipimo visipatikane na madawa hayo yaliyopigwa marufuku.

No comments:

Post a Comment