Thursday, 21 July 2016
Kocha mkuu wa Yanga Pluijim ameongezewa mkataba wa miaka miwili
Na Chrispino Mpinge
Yanga imefanikiwa kumaliza utata wa kuendelea na kocha wao kocha baada ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili.
Mkataba wa Pluijm na Yanga ulifikia tamati mwezi mmoja uliopita ambao ndiyo umeipa klabu hiyo mafanikio ya kutwaa taji la ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara mara mbili, Kombe la FA pamoja na kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.
Kocha Pluijm amesema anafuraha ya kuendelea kuifundisha Yanga ambapo sasa anataka kuhakikisha anaendeleza kazi na mafanikio zaidi kwa Yanga kuweza kufika mbali katika mashindano ya CAF mwakani.
Pluijm amesema, anaipenda Yanga na sikuzote amekuwa akifanya kazi kwa kutanguliza heshima.
Pluijm amesema, changamoto yake kubwa kwa sasa ni kuhakikisha Yanga inafanya vizuri zaidi japo haitakuwa kazi rahisi.
Mkataba huo wa Pluijm ambaye wikiendi iliyopita aliibuka kuwa kocha bora wa msimu uliopita ameusaini mbele ya katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit.
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment