Mchungaji Feki na Waombewaji wawekwa Mikononi mwa Polisi DSM
Anayejiita mchungaji David Mwamkinga amejikuta mikononi mwa polisi
jijini Dar es Salaam baada ya ndugu wa baadhi ya wafuasi wa mchungaji
huyo kuamua kuwatoa ndugu zao waliofungiwa ndani kwa zaidi ya miaka 10 ,
kwa lengo la kufanyiwa maombi kutokana na maradhi yanawasumbua.
Hatua hiyo inafuatia kilichoelezewa kuwa ni kuzidi kudhoofika kwa hali
za waombewaji hao ambapo jeshi la polisi limeingilia kati na kufanikiwa
kumkamata mchungaji huyo pamoja na wafuasi wake eneo la Magomeni Kagera
na kuelekea nao kituoni.
No comments:
Post a Comment