Baadhi ya mashtaka yanahusu mkataba wa ununuzi wa silaha
Waendesha mashtaka
nchini Afrika Kusini wanatarajiwa kufichua leo iwapo watafufua mamia ya
mashtaka ya ulaji rushwa dhidi ya Rais Jacob Zuma
Hii ni
kufuatia uamuzi wa mahakama mwezi jana ambayo ilisema uamuzi wa
kutupilia mbali mashtaka hayo haukuwa wa busara na unafaa kutafakariwa
upya.
Maelfu waandamana kupinga utawala wa Zuma
Zuma akubali makosa kuhusu ukarabati Nkandla
Mashtaka hayo yanajumuisha kashfa kubwa ya mabilioni ya dola ya ununuzi wa silaha iliyofutiliwa mbali mwaka 2009.
Zuma amekabiliwa na shinikizo za kumtaka ajiuzulu
Kufutiliwa mbali kwa mashtaka hayo kulimfungulia njia Bw Zuma kushinda urais wiki chache baadaye. Wachanganuzi
wa masuala ya kisiasa wanasema iwapo mashtaka hayo yatafufuliwa, basi
hatua hiyo itaongoeza shinikizo za kumtaka Bw Zuma ajiuzulu.
No comments:
Post a Comment