Friday, 20 May 2016

Waziri wa Ulinzi wa Israel Moshe amejiuzulu

 Ya'alon
Bw Ya'alon amesema Israel imepoteza mwelekeo
Waziri wa Ulinzi wa Israel amejiuzulu akisema hana imani na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

 

Bw Moshe Ya'alon ametangaza kujiuzulu kwake kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
Aidha, amesema ataacha kujihusisha na siasa.

Kumekuwa na taarifa kwamba Bw Netanyahu, anapanga kukaribisha chama chenye msimamo mkali kinachoongozwa na Avigdor Lieberman kwenye muungano wake unaotawala.

Bw Lieberman aliwahi kuhudumu kama waziri wa mambo ya nje na anajulikana kwa kutoa matamshi makali na kuwa na msimamo mkali dhidi ya Wapalestina.

Awali Alhamisi, Bw Ya'alon aliwahutubia viongozi vijana wa Israel na kusema taifa hilo limepoteza mwelekeo wake kimaadili.

Taarifa katika vyombo vya habari nchini Israel zinasema Bw Netanyahu atamteua Bw Lieberman kuwa waziri mpya wa ulinzi.


 Netanyahu



Bw Netanyahu na Bw Lieberman
Bw Lieberman alijiuzulu 2012 baada ya uchunguzi kuhusu ukosefu wa uaminifu kuanzishwa Dhidi yake yake.
Alishtakiwa lakini baadaye akapatikana bila hatia.

No comments:

Post a Comment