Friday, 20 May 2016

Bendera na Wimbo maalumu zitaanza kutumika katika taasisi na idara za Serikali za nchi Wanachama

 
Alama za Jumuia ya Afrika Mashariki ikiwemo Bendera na wimbo maalumu zitaanza kutumika katika taasisi na idara za serikali za nchi wanachama.

 

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mkataba wa uanzishwaji wake.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, Mindi Kasiga, kuanzia ngazi ya chini kwenye serikali za mitaa ambako bendera ya taifa inapepea ni lazima ya jumuia hiyo iwepo.

Aidha amesema pia kwenye shughuli rasmi za serikali, wimbo wa taifa unapoimbwa ni lazima pia wa Afrika mashariki uimbwe pia.

Jumuia ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya Burundi, Rwanda, Sudan Kusini.

No comments:

Post a Comment