Na Mwandishi Wetu
Watanzania
ambao wanapenda kutembelea nchi ya Uingereza wametakiwa kuzingatia
taratibu zilizowekwa na nchi hiyo katika maombi ya viza ikiwemo kuomba
viza mapema, kuwasilisha nyaraka zote muhimu pamoja na taarifa sahihi
ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.
Ushauri huo umetolewa leo
Bungeni Dodoma na Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe.
William Ole Nasha ambaye alijibu swali kwa niaba ya Waziri mwenye
dhamana katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga lililotaka kujua
ni sababu zipi zinazoifanya Serikali ya Tanzania iridhike na utaratibu
unaoleta usumbufu kwa Watanzania wanaotaka kusafiri kwenda Uingereza
kutafuta viza kupitia Kenya na Afrika Kusini.
Mhe. Ole Nasha ameeleza kuwa,
hapo awali huduma za viza zilikuwa zikitolewa na Ubalozi wa Uingereza
nchini, Ubalozi huo ulihamisha shughuli za utoaji wa viza kutoka hapa
nchini kwenda nchini Kenya tarehe 1 Desemba, 2008 na kuanzia tarehe 18
Agosti, 2014 huduma hizo zimehamishiwa nchini Afrika Kusini na siyo
Kenya tena.
Alifafanua kuwa, kwa mujibu wa
Serikali ya Uingereza uamuzi huo ni wa kisera ba umefikiwa ili kuleta
ufanisi katika utendaji kazi wa Idara ya Viza na Masuala ya Uhamiaji ya
Uingereza.
“Mchakato wa utoaji viza za
Uingereza unafanyika Kikanda, kwa mantiki hiyo maombi yote ya viza
kutoka nchi zote za Afrika Mashariki na Kati yanafanyiwa kazi katika
Ubalozi wa Uingereza nchini Afrika Kusini”, alisema Ole Nasha.
Aidha, Waombaji wa viza hapa
nchini wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja na nyaraka
zinazohitajika katika Kituo cha Kuombea Viza (Visa Application Centre)
kilichopo Viva Tower, Dar es Salaam.
“Kituo hicho ndicho chenye
jukumu la kusafirisha maombi hayo kwenda Afrika Kusini na kurejesha
nyaraka husika kwa waombaji nchini, Mwombaji halazimiki kufuata huduma
hiyo nchini Afrika Kusini”, alisema Mhe. Ole Nasha.
Amefafanua kuwa, Ubalozi wa
Uingereza Nairobi unashughulikia maombi machache ya viza (restricted
number of applications) kwa Viongozi wa Serikali na watendaji wengine
wenye pasi za Kidiplomasia hasa katika hali ya dharura ambapo maombi
hayo yanapaswa kupelekwa moja kwa moja Ubalozi wa Uingereza Nairobi na
waombaji wenyewe au kupitia Ubalozi wa Tanzania Nairobi.
“Napenda
kuwakumbusha Waheshimiwa Wabunge pamoja na Watanzania wenzangu kwamba.
Zoezi la utoaji viza lina utaratibu Wake na moja ya taratibu hizo ni
kwamba nchi inayotoa Viza Ina Uluru wa kuamua ni wapi itatolea viza
hizo, kwa mantiki hiyo hata Serikali yetu ya Tanzania ku pitia Balozi
zake zilizopo nje inazo taratibu zake za kutoa viza kwa wageni wote
wanaotembelea Tanzania, ni vema Watanzania ambro wangependa kutembelea
nchi ya Uingereza wakazingatia taratibu zilizowekwa na nchi hiyo katika
maombi ya viza”, alisisitiza Ole Nasha.
No comments:
Post a Comment