Tuesday, 3 May 2016

Umoja wa Mataifa Umempongeza Rais John Pombe Magufuli Kudhibiti Rushwa Nchini


 
 Na Mwandishi Wetu

Umoja wa Mataifa ya Ulaya umepongeza Hatua zinazochukuliwa na Rais Dkt. John Magufuli,katika kudhibiti Vitendo vya Rushwa nchini na kuahidi kutoa Misaada zaidi ili kuboresha Huduma za kijamii na kiuchumi.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Mwanza na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguezi,pamoja na Mkuu wa idara ya Siasa na Mawasiliano wa Umoja wa Ulaya alipomtembelea Wa mkoa wa Mwanza John Mongella.

Pamoja na mambo mengine Umoja huo wa Ulaya Umetembelea Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuangalia fursa za Uwekezaji ambapo umeiomba Serikali ya Tanzania kuondoa Urasimu katika Upatikanaji wa vibali vya Uwekezaji.

Licha ya Kupongeza hatua hizo za Rais John Magufuli katika kupambana na Rushwa Ujumbe huo wa Umoja wa ulaya Umetaka Serikali iweze kuchukua Hatua Zaidi Dhidi ya wale wote Watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo Vya Rushwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza katika kuchangamkia Fursa za Miradi inayofadhiliwa na Umoja huo lakini pia ni njia moja wapo ya kudumisha mahusiano ya Kimataifa.

Ujumbe huo Umetembelea Baadhi ya Miradi Wanayoifadhili mkoani humo ikiwemo Mradi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza Pamoja na Mradi wa kuongeza thamani ya ngozi katika chuo cha Teknolojia DIT tawi la Mwanza

No comments:

Post a Comment