Mtaalam
wa upasuaji wa mfumo wa neva (neurosurgeon) Sergio Canavero kutoka
nchini Italia, anakusudia kufanya Jaribio la kwanza la kupandikiza
kichwa cha binadamu kwenye mwili wa Binadamu Mwingine, ifikapo mwakani.
Wataalam
wengi wa Upasuaji Wanafikiria wazo hilo ni la kiuwendawazimu, lakini
sio kwa mtaalamu huyo, kwani anasema Bado anapanga kujaribu pandikizo la
kwanza la kichwa kwa binaadamu. (Head Transplant)
Dk.
Canavero ambaye mpaka sasa ameshapata mtu wa kujitolea kufanya zoezi
hilo, kijana mwenye asili ya Urusi ambaye ni mtaalam Wa software Valery
Spiridonov, ambaye ana tatizo la kupoteza nguvu kwa misuli yake ya
mwili.
Dk.
Canavero amesema mafanikio yake yameonesha kuwa mpango Wake wa
kupandikiza kichwa cha binadamu kwa mwili wa mtoaji (Donor) Bado upo, na
ataanza Mpango huo Mwishoni Mwa Mwaka 2017 na unaweza kuwa njia ya
kutibu waliopooza Mwili.
“Ningesema
tuna Takwimu nyingi Zinaendelea, ni Muhimu kwa watu kuacha kufikiria Jambo hili sio Rahisi, hii inawezekana kabisa na Tunaendelea kulifanyia
kazi”, alisikika Dk, Canavero akimwambia Mwanasayansi mchanga.
Timu
iliyo nyuma ya kazi hiyo ilipost video ikimuonesha nyani ambaye Alifanyiwa upandikizwaji huo, na kufanikiwa kutembea Baada ya uti Wa
mgongo kutenganishwa na kuunganishwa tena'
Upandikizwaji
wa kichwa kwa nyani ulifanywa katika chuo cha Harbin Nchini China (
Harbin Medical University) na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, bila kuwa na
muathiriko wowote katika uti wa mgongo,
lakini aliuawa Baada ya Masaa
20 Baadaye, kutokana na sheria za kazi.
Dk.
Canavero amesema atahitaji Pesa nyingi ili kuwalipa Timu ya Upasuaji,
kwa mtu wa kwanza ambaye ni Raia wa Urusi, hivyo Amemuomba Mwanasayansi
tajiri zaidi Mark Zuckerberg, kufadhili Upasuaji huo.
No comments:
Post a Comment