Siku
moja baada ya serikali kuziagiza mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya
Mapato Tanzania-TRA, kufanya Uchambuzi wa kina ili kubaini Sababu za
kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya
Dar es salaam kwenda nchi jirani, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA) Injinia Alois Matei, leo amejitokeza Mbele ya waandishi wa habari ili kutaja chanzo cha mizigo kupungua Bandarini.
Agizo la kuzitaka mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi huo lilitolewa juzi Bungeni April 30 na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dr. Philip Mpango .
Dr
Mpango alisema katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana na Machi Mwaka huu kontena zilizopelekwa nchini Congo zilishuka kutoka 5,529 hadi
4,092, wakati yale yaliyokuwa yakipelekwa nchini Malawi yalishuka
kutoka kontena 337 hadi 265, huku yale ya Zambia yakishuka kutoka 6,859
hadi kufikia 4,448, hivyo
akaziagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA na Mamlaka ya Mapato-TRA,
zichambue mwenendo huo ili kubaini chanzo cha kupungua.
Akiongea
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Alois Matei amesema sababu
kubwa ya kupungua kwa makontena hayo imesababishwa na kuyumba kwa
uchumi wa dunia hasa China na kwingineko ambako mizigo inayopitia
bandari ya Dar es Saam hutoka.
“Biashara
za bandari dunia nzima zimeshuka.Kipindi hiki kuna mtikisiko kidogo
kutokana na uchumi wa dunia kuyumba hasa China na kwingineko.
"Juzi
tuliongea na wenzetu wa Singapore ambao walikuja hapa nchini, nchi yao
ni moja ya nchi inayofanya biashara ya bandari kwa kiasi kikubwa. Wao
pia walisema wamekumbana na tatizo hilo la kushuka kwa mizigo katika
kipindi cha hii miezi mitatu." Amesema Matei
Katika hatua nyingine, Injinia Matei amesema serikali
imepanga kutumia Dola milioni 690 kuimarisha miundombinu ya Bandari ya
Dar es Salaam ili kuongeza uwezo wa kupokea mizigo hadi kufikia tani
milioni 38 ifikapo 2030 kutoka tani milioni 16 za mwaka 2014/15.
Akifafanua kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Matei
amesema mradi huo Unatekelezwa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia,Trade
Mark East Africa na DFID na unatarajia kuanza kabla ya mwisho wa
mwaka 2016.
“Serikali,Benki
ya Dunia,Trade Mark East Africa na DFID zimetiliana saini makubaliano
ya ushirikiano wa utekelezaji wa mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es
Salaam” alisisitiza Matei.
Akizungumazia
maeneo yatakayohusika katika maboresho hayo Injinia Matei amesema kuwa
yatahusisha Uboreshaji na uongezaji wa kina kufikia Mita 14 katika gati
namba 1 hadi 7 ili kuwezesha meli kubwa zaidi kutia nanga.
Maeneo
mengine ni ujenzi wa gati mpya ya kushushia magari katika eneo la
Gerezani Creek, uchimbaji ili kuongeza kina cha lango la kuingilia meli
hadi kufikia mita 14 pamoja na sehemu ya kugeuzia meli.
Eneo
jingine ni uhamishaji wa gati la mafuta la Koj pamoja na bomba la Mafuta katika eneo la ujenzi, uboreshaji wa mtandao wa reli ndani ya Bandari na ujenzi wa sehemu ya kupakilia na kushushia mizigo.
Mhandisi
Mkuu wa TPA Bi Mary Mhayaya akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa Flow
meter mpya ya Kigamboni ambao umeshakamilika na hivyo kuwezesha mafuta
yote yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam kupimwa na
kujulikana kiasi halisi kilichoingizwa hapa nchini ili kuiwezesha
Serikali kupata mapato stahiki ikiwemo kodi
No comments:
Post a Comment