Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
Serikali za Vijiji nchini
zimekumbushwa kusimamia vizuri Sheria ya Ardhi Na. 5 ya mwaka 1999
ambayo imeweka utaratibu wa kufuata kwa mtu anayehitaji kupata ardhi kwa
matumizi mbalimbali.
Agizo hilo limetolewa leo
Bungeni Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa
Jimbo la Chemba,
Mhe. Juma Nkamia ambaye alitaka kujua utayari wa Serikali wa kufuta uamuzi uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara wa kuwazuia wakulima ili kuondoa mgogoro wa muda mrefu.
Mhe. Juma Nkamia ambaye alitaka kujua utayari wa Serikali wa kufuta uamuzi uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara wa kuwazuia wakulima ili kuondoa mgogoro wa muda mrefu.
Mhe. Jafo ameeleza kuwa, tamko
lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara liliwahusu wakulima waliokuwa
wavamizi katika eneo la hifadhi ya Wanyamapori ya Makame kutoka katika
Wilaya za Kiteto, Babati, Chemba, Kondoa na Mkoa wa Iringa waliokuwa
wanaendesha shughuli za kilimoi katioka hifadhi hiyo kinyume cha Sheria.
Amefafanua kuwa, uamuzi huo
ulitolewa kufuatia azimio la kikao cha pamoja cha Kamati za Ulinzi na
Usalama za Wilaya za Kiteto cha Chemba kilichokaa tarehe 12 Novemba,
2015.
“Kikao hicho kilishirikisha
viongozi wa Vijiji vitano vinavyounda Mamlaka ya Hifadhi (WMA) ambavyo
ni Ngobolo, Katikati, Ndedo, Irkiushbor na Makame pamoja na wawakilishi
wa wakulima 10 kutoka kila Wilaya”, alisema Mhe. Jafo.
Aidha, kwa mujibu wa Sheria,
hairuhusu shughuli yoyote ya kibinadamu ikiwemo kilimo, ufugaji au
makazi kuendeshwa katika hifadhi.
“Naomba kutoa wito kwa wananchi
kuzingatia Sheria za nchi ili kuepuka migogoro katika jamii, Serikali za
vijiji zinakumbushwa kusimamia vizuri Sheria ya Ardhi Na. 5 ya mwaka
1999 ambayo imeweka utaratibu wa kufuata kwa mtu anayehitaji kupata
ardhi kwa matumizi mbalimbali, lengo ni kuzuia migogoro ya ardhi
isiyokuwa ya lazima ambayo kwa sehemu kubwa inatokana na kutozingatiwa
kwa Sheria za ardhi”, alisema Mhe. Jafo.
No comments:
Post a Comment