Mkurugenzi
Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho akifungua mkutano
wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya
vijana leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi
ya vijana na wadau wa vijana akifuatilia kwa makini mada zilizokua
zikiendelea wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana
kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Dkt. Abdallah Possi akizungumza na vijana na wadau wa vijana
(hawapo pichani) wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya
vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho
(kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi wakati wa
mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala
mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
Vijana
wanaoishi kwa matumaini wakitoa nasaha kwa vijana wengine jinsi ya
kujitunza na kufikia malengo waliyojiwekea wakati wa mkutano wa mwaka wa
wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo
Jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Kilimanjaro marathoni changia dola elfu tano kuondoa unyanyapaa,
maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na vifo vitokanavyo na ukimwi Bw.
Mrisho Mpoto akiteta jambo na vijana jinsi ya kupambana na VVU leo
jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya
vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa
masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar
es Salaam
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Dkt. Abdallah Possi (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja
na viongozi na vijana walioshiriki katika mkutano wa mwaka wa wadau wa
masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo jijini Dar
es Salaam. Wanne kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi
Bibi. Fatma Mrisho
.
Na: Golden Mwakatobe
Serikali imedhamiria kuhakikisha
kuwa vijana wote nchini wanashirikishwa kikamilifu na kupatiwa huduma
zinazotakiwa ili kumaliza uwepo wa maambukizi mapya ya virusi vya
ukimwi, kupunguza ubaguzi na unyanyapaa unaotokana na ukimwi pamoja na
kupunguza vifo vitokanavyo na ukimwi kwa vijana.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt.
Abdallah Possi alipokua akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala
ya vijana leo Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Possi amesema kuwa asilimia 2
ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yapo miongoni mwa vijana wenye
umri kati ya miaka 15 hadi 24 ambapo ushamiri kwa vijana wa kike uko
juu zaidi ya ule wa vijana wa kiume hasa katika umri wa miaka 23 hadi
24.
Akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi Mtendaji Tume ya kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho amesema
kuwa Tume inaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa watoto na
vijana wanapata kinga na huduma stahiki kupunguza utegemezi hivyo
kuwafanya vijana kujiamini na kujitokeza kupambana na VVU/UKIMWI
“Vijana ni nguvu kazi ya taifa la
leo, wakipatiwa nafasi ya kujitambua na kuwasilisha hisia zao utegemezi
ndani yao utapungua, ni vyema vijana wakaandaliwa mazingira ambayo
watakua huru kushiriki katika masuala ya VVU na UKIMWI” Alisema Bibi.
Mrisho.
Aidha Bibi. Mshiro amemtaka kila
kijana aliyeshiriki mkutano huo kubeba mambo muhimu manne na
kuwafikishia vijana wengine kumi waliopo vijiweni, maofisini ama sehemu
nyingine yeyote ile ili kuweza kusambaza elimu waliyoipata kwa kila
kijana nchi nzima na kuokoa afya za vijana wenzao.
Kwa upande wake kijana anayeishi
kwa matumaini Bi. Wittiness Nakanje ameiomba serikali kuanzisha kliniki
maalumu za vijana wanaoishi na VVU/UKIMWI ili kuwaweka vijana kuwa huru
kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata elimu ya VVU na UKIMWI.
Kulingana na utafiti wa viashiria
vya UKIMWI kwa mwaka 2011/2012 tanzania inajumla ya vijana milioni 12
wa umri wa 10 hadi 19 ikiwa ni asilimia 24 na milioni 16 wa umri wa
miaka 19 hadi 24 ikiwa ni asilimia 24 ya Watanzania wapatao milioni 44,
idadi hiyo ya vijana inajumuisha wasichana wapatao 7,430,840 na wavulana
6,924,612.
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na
makazi ya mwaka 2012 vijana wa umri wa miaka 19 hadi 24 wako 3, 954,039
ambapo wasichana idadi yao ni 2,160,986 sawa na asilimia 55 na wavulana
1,793,053 sawa na asilimia 45.
No comments:
Post a Comment