Na Mwandishi wetu
Serikali
inaendelea na mazungumzo na wawekezaji wanaokusudia kuwekeza katika
viwanda vya sukari ili kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya
kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini.
Kauli hiyo
imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati
akijibu maswali ya papo kwa papo ya kila Alhamis.
Alisema kuwa
lengo la mazungumzo ya kutaka viwanda viweze kuongeza uzalishaji wa
sukari ili uweze kufikia tani 420,000 katika kipindi miaka minne ijayo
na hivyo kupunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.
Mhe.
Majaliwa alisema kuwa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa
viwanda vipya ya Sukari ni pamoja na Kigoma, Morogoro na Bonde la Rubada
lilipo katika mto Rufiji.
Kuhusu
kutojengwa kiwanda cha Sukari katika eneo la Bagamoyo , Waziri Mkuu
alisema kuwa Serikali ilikataa kuruhusu ujenzi wa kiwanda cha Sukari
katika eneo hilo baada ya Kamati ya Bunge kushauri kuwa kisijengwe kwa
sababu kingehatarisha uhai wa wanyama waliomo katika Mbuga ya Saadan kwa
kuwa kingetumia maji mengi kutoka Mto Wami.
Mhe.
Majaliwa alisema kuwa hali hiyo ingesababisha upungufu wa maji ambayo
ni tegemeo kwa wanyama wa Mbuga ya Saadan yambao ni muhimu kwa sekta ya
utalii nchini.
Kwa upande wa upungufu wa sukari nchini , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imeagiza tani 70,000 kutoka nje ya nchi.
Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.
Mhe.
Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo
imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa Sukari
nje wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na hivyo
kuathiri viwanda vya hapa nchini.
Aliongeza
kuwa Bodi hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini (TRA )
itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini ndio
inayohitajika.
Kuhusu bei elekezi ya sukari , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi wa kawaida.
Alisema kuwa bei hiyo zinazingatia gharama zote ikiwemo usafirishaji kuto

Alisema kuwa bei hiyo zinazingatia gharama zote ikiwemo usafirishaji kuto ka zinapoagizwa na kumfikia mlaji.
No comments:
Post a Comment