Rais wa Rwanda Paul
Kagame amekana madai yaliotolewa na Umoja wa Mataifa kwamba Taifa lake
linaendelea kuwasaidia waasi katika nchi jirani ya Burundi.
Burundi imekabiliwa na mgogoro mbaya wa kisiasa tangu rais Pierre Nkurunziza kuamua kupigania muhula mwengine mwaka uliopita.
Ni mwaka mmoja kamili tangu Rais Nkurunziza kuepekua jaribio la mapinduzi.
Rwanda ilikana madai kama hayo kuhusu kuwaunga mkono waasi katika ripoti ya awali ya Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Februari.
Bw Kagame amekosoa wachapishaji wa ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baadaye,ikisema mda wake ungetumika vyema kuangazia matatizo yanayokumba mataifa badala ya kuyazidisha.
Ripoti hiyo iliopatikana na chombo cha habari cha Reuters imeishtumu Rwanda kwa kutoa Mafunzo pamoja na usaidizi wa kifedha kipindi chote cha mwaka 2016 kwa waasi wanaolenga kumuondoa madarakani rais Pierre Nkurunziza.
No comments:
Post a Comment