Afisa wa ukaguzi
katika shirikisho la soka duniani Fifa Domenico Scala,amejiuzulu
akipinga Mabadiliko yanayofanyika katika shirikisho hilo.
Baraza hilo lilichukua mahala pa kamati kuu ya Fifa kufuatia madai ya ufisadi katika shirikisho hilo.
''Kamati hizo sasa zitakuwa hazina uhuru kutekeleza majukumu yake'',alisema Scala.
Ameongezea kuwa: Hatua hiyo inahujumu nguzo ya uongozi mzuri wa Fifa na inaharibu ufanisi wa mabadiliko yaliofanywa.
Scala alikuwa na jukumu muhimu katika kusukuma mabadiliko kufuatia kashfa iliolazimu kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter na mwenzake wa Uefa Michel Platini.
No comments:
Post a Comment