Rais wa Venezuella Nicolas Maduro amejiongezea mamlaka
Rais Nicolas Maduro wa Venezuella
Rais wa Venezuella,
Nicolas Maduro, amesema yuko tayari kuongeza mamlaka yake chini ya Utawala wa hali ya hatari iliyotangazwa wiki iliyopita.
Hatua hiyo
imefikiwa ili kukabiliana na waandamanaji wanaopinga serikali ya taifa
hilo. Maduro amedai kuwa upinzani unachochea ghasia na pia kupanga njama
ya kuipindua Serikali yake. Amesema hatasita kuchukua hatua zinazofaa
ili kudumisha amani nchini Venezuela, ambayo inakabiliwa na mzozo mkubwa
wa kiuchumi.
No comments:
Post a Comment