Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
amesema kuwa serikali yake imepigwa na butwaa na Matamshi ya kushtua na
ya aibu ya waziri mkuu wa Uingereza Bw David Cameron yakwamba Nigeria na
Afghanistan ndio mataifa fisadi zaidi duniani.
Rais Buhari akizungumza kupitia msemaji wake, Garba Shehu ametaja matamshi ya Cameron kuwa ya aibu na kushtua.
”Kiongozi huyo wa Nigeria anasema labda Cameron alikuwa akizungumzia utawala uliondoka Madarakani mwezi Mei mwaka uliopita wa aliyekuwa Rais Goodluck Jonathan.
”Buhari alichaguliwa kwa jukwaa la kupamabana na ufisadi.”
”yeye ndiye kifagio cha ufisadi nchini Nigeria.”
No comments:
Post a Comment