Amir Khan azidi kujitetea katika Pambano lake
Bondia Amir Khan amesema hakuna
uwezekano wowote wa yeye kuchuana na mpinzani wake Mkuu Kell Brook,
licha ya kushindwa vibaya na Saul Canelo Alvarez.
Kulikuwa na matumaini makubwa kuwa
kufuatia uamuzi wake wa kujiunga katika uzani wa Kati au Middleweight,
pambano kati yake na bingwa wa shirisho la kimataifa la dondi IBF, Kell
Brook, lingeandaliwa. Lakini Khan amesema Brook sio bondia mwenye
tajiriba na kwa Sasa hawezi kushiriki pigano lolote dhidi yake.
Amesema anamheshimu bondia huyo, kwa
sababu ni bingwa wa dunia lakini tofauti zao Haziwezi kumruhusu kukubali
kupambana naye. ”Ningependa kupambana na mabondia Mashuhuri duniani,
ili kuwa na rekodi nzuri na kwa sasa nimesalia na mapambano machache tu”
Alisema Khan.
Khan anayetoka eneo la Bolton na Brook
kutoka Sheffield wamekuwa wakitaniana kwa muda Na wakati Brook
aliposhinda taji la dunia kulikuwa na dalili ya pambano lao kufuata
lakini Sasa Khan hayupo tayari.
No comments:
Post a Comment