Kamanda
wa Polisi kanda maaalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro akionesha
waandishi wa habari mzani unaodaiwa kutumiwa na tapeli wa madini kupima
madini bandia na kuwatapeli wananchi wakati wa kutoa taarifa ya
kukamatwa kwa tapeli huyo Jijini Dar es salaam Mei 20 2016.
Na Raymond Mushumbusi
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam limemkamata mtuhumiwa anayejulika kwa jina la Wenceslaus
Mtui(46) mkazi wa Makongo Juu kwa kosa la utapeli wa sh. Milioni 90 .
Akizungumza na waandishi wa
habari leo Jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi kanda maaalum ya Dar
es Salaam Kamishna Simon Sirro amesema wamefanikiwa kumkamata tapeli
huyo mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa Bw. Kelvin Nyerere(26)
mkazi wa Msasani ambaye alishawishiwa na kutapeliwa kwa kuuziwa madini
bandia na mtuhumiwa huyo.
Kwa mujibu wa kamanda Sirro,
mtuhumiwa huyo alikamatwa mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa
Nyerere aliyetapeliwa, askari walifika eneo la tukio na kumkamata
mtuhumiwa na kumfikisha kituo cha polisi kwa mahojiano.
Aidha baada ya kufanyika kwa
upekuzi ofisini na nyumbani kwa mtuhumiwa, kulikutwa na vitu
vilivyodhaniwa kuwa ni madini, chuma cha kuchomea madini, mashine ya
kupimia madini, vifaa vya kubania madini (53), mashine ya kupimia
madini, nyaraka za kuwekea fedha kutoka Benki mbalimbali na hati za
usajili wa makampuni ambazo zilitiliwa shaka.Vielelezo vyote
vilichukuliwa kwa uchunguzi.
Mtuhumiwa huyo bado anashikiliwa
na Jeshi la Polisi upepelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani
kujibu tuhuma zinazomkabili za kufanya utapeli wa kuuza madini bandia
ambayo ni kinyume cha Sheria za nchi.
Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa
watu wanaojifanya wafanyabiashara wa madini kuacha mara moja tabia hiyo
na wananchi wanaohitaji kununua madini wafike Ofisi za Wakala wa
Madini(TMAA) ili kuepukana na matapeli.
No comments:
Post a Comment