Jeshi
la polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa
chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold
Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi
dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi
Davis Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya
viongozi hao.
Akiongelea
tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa
tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu majira ya saa 09:00 asubuhi .
Alisema
kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi
ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa
haiwezekani viongozi wote wawe nje ya nchi huku akuna kiongozi aliyepewa
mamlaka ya kukikaimu kiti.
“Mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya ,Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti,hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema Mkumbo.
Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtumiwa huyo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo,”Dr
Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji
ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa
watawala na sio wananchi wa kawaida hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama facebook."
Mkumbo
alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi
utakapo kamilika,huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya
kijamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka sheria na
taratiu za kisheria .
Alitumia
muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika anatumia
mitandao vibaya na kusema kuwa atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi
yake.
Wakati
hayo yakiendelea mshtakiwa wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya
muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Isaac Emily (40), mkazi wa
Olasiti jiji hapa inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5
mwaka huu katika mahakama ya hakiku mkazi Arusha.
No comments:
Post a Comment